published on in blog

Shirika la kitaifa la uchukuzi Kenya latazamiwa kuzindua safari za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi

- Shirika la uchukuzi la Kenya (KQ) linatarajiwa kuzindua safari za ndege za moja kwa moja kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy (JFK)

- KQ itakuwa ikisafiri moja kwa moja kutoka Nairobi hadi New York kuanzia Oktoba 2018, hivyo kupunguza muda wa usafiri kati ya miji hiyo miwili kutoka saa 22 hadi saa 15

- Wanaopanga kusafiri wanatarajiwa kuhifadhi nafasi mapema huku KQ ikijiandaa kufanya safari yake ya kwanza Amerika

Habari njema huku shirika la uchukuzi la kitaifa, Kenya Airways (KQ), likijiandaa kuanza safari za moja kwa moja kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy (JFK) mjini New York.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Akithibitisha ratiba mpya za safari hizo mnamo Jumanne, Januari 10, mwenyekiti wa Kenya Airway, Michael Joseph, alisema wataanza rasmi safari mnamo Oktoba mwaka huu.

Kulingana na bosi wa KQ, tayari wamepakia ratiba mpya za usafiri katika mfumo wao na wasafiri wanaweza kuanza kuhifadhi nafasi.

Habari Nyingine: Fahamu jinsi wauzaji wa nguo Gikomba huwaibia wateja wao baada ya kulipwa (video)

Habari Nyingine: Mkenya wa kwanza seneta Australia azuru nchini na kutekeleza jambo la kushtua

Wanaopanga kusafiri wanatarajiwa kulipia mapema ili kujiandaa kwa safari ya kwanza kabisa ya moja kwa moja hadi Amerika.

Shirika hilo la uchukuzi litakuwa likisafiri moja kwa moja kutoka Nairobi hadi mjini New York. Hii inatarajiwa kupunguza mno muda wa safari kati ya miji hiyo miwili kutoka zaidi ya saa 22 hadi saa 15.

Habari Nyingine: Limousine ya KSh208 M iliyo na uwezo wa kwenda ardhini na majini (Picha)

Kulingana na maafisa wa shirika hilo, tayari wametengewa nafasi ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy.

KQ itakuwa ikiondoka JKIA saa 10.30 asubuhi kila siku. Itatua New York siku inayofuata saa 6.30 asubuhi.

Wanaorejea kutoka New York kuelekea Nairobi wataondoka saa 1.30 adhuhuri na kutua JKIA saa 10.30 asubuhi siku inayofuata.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia394gpNmqqGhop64onnLmmSkoaSWtqetjKWYZq2TncKswdmiZKSdnq6ubrjArZizmZ2exKJ5yq6xoqaUqq5uv8CfmKuhXa%2BubrnOo5hmo6eWeq67yZpkpK2kpLiiec2aoKunkp56qa3DomSnnadixrC%2BymefraWc