published on in blog

Mke avunja ndoa kwa ulevi

Wakazi walishuhudia sinema ya bure katika mtaa wa Tawa, Mbooni pale ambapo jamaa alimtimua mkewe kwa kufika nyumbani akiwa amelewa chakari.

Penyenye zinaarifu kwamba, mwanamke huyo alikuwa na mazoea ya kubugia pombe kisiri wakati mumewe akiwa kazini.

Habari Nyingine: Mwea: Mama asutwa kwa kutaka mabinti zake wawe na masponsa

Kwa mujibu wa Taifa Leo, siku ya kisanga mama huyo alishinda klabuni akinywa pombe na wenzake pasi na kujua kilichomsubiri.

Inaarifiwa kwamba mumewe alianza kumshuku pale ambapo alikataa kupokea simu na ikamlazimu kufunga safari ghafla kutoka jijini kuelekea nyumbani kubaini kilichojiri.

Jamaa alifika nyumbani na kuanza kuingia na wasiwasi kwani hata baada ya saa mbili alizomsubiri mkewe nyumbani, hakuona dalili zozote zake kuwasili huku mama huyo akiendelea kudinda kupokea simu zake.

Jioni, mama huyo alifika nyumbani akiwa amelewa chakari na kumfanya mumewe kupigwa na butwa kumsikia akiropokwa maneno yasiyokuwa yakieleweka.

Duru zinaarifu kwamba, kwa hasira jamaa alitoka nje na kuanza kumzomea mkewe.

"Tabia ya ulevi ulianza lini? Mimi mwenyewe sinywi pombe, wewe ni nani kunywa pombe. Rudi huko ulikotoka ukaendelee kunywa pombe," jamaa alisikika akimfokea mkewe.

Inasemekana kipusa huyo alijaribu kusimama wima kumshawishi mumewe kwamba hakuwa mlevi ila juhudi zake ziliambulia patupu.

Habari Nyingine: Zlatan Ibrahimovic: Nyota wa LA Galaxy kupigwa marufuku kwa kumsababishia mpinzani jeraha linalohitaji upasuaji

"Hapa ni kwangu na siwezi nikakuruhusu unywe pombe. Leo nimekupata vizuri hauna bahati. Kwenda kabisa," jamaa alizidi kuwaka.

Mama kuona taabu iliyomfika alianza kumuomba mumewe msamaha huku akiapa kutorudia tena.

Hata hivyo, jamaa huyo ambaye alikuwa amepandwa na mori ajabu alimpuuza na kumuamuru aondoke mara moja kabla amuonesha cha mtema kuni.

Inasemekana mwanadada alipodinda kuondoka, mumewe aliingia chumbani akachukua nyahunyo na kumtimua huku akiapa kutorudiana na yeye tena.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZn5xgZFmpKSdXZbDtrrJmmSnnJ%2BWeqzDwGaspZ2mnnupwMyl